Deni la ushuru Sh14 bilioni lazidi kumsakama Seneta Karanja
SENETA wa Nakuru Tabitha Karanja, ambaye pia ni mwanabiashara na mmiliki wa kampuni ya kutengeneza pombe ya Keroche Breweries Limited, amepewa muda wa mwezi mmoja kulipa mamlaka ya ushuru nchini (KRA) Sh14bilioni alizokwepa kulipa.
Hakimu Mwandamizi wa Mahakama ya Milimani Bw Geoffrey Onsarigo alimpa Bi Karanja muda huo baada ya kuelezwa na wakili wake kwamba “mashauri ya kusuluhisha suala hilo la ushuru ambao Kerocho ilikwepa kulipa yamo kileleni sasa.”
Mahakama ilikabidhiwa barua jinsi KRA na Keroche zimeafikiana.
Mahakama ilielezwa kwamba sheria inapendekeza mashauriano yapewe kipaumbele.
Bi Karanja ameshtakiwa kwa kukwepa kulipa ushuru wa Sh14.5 bilioni.
Amekanusha mashtaka 10 dhidi yake na yuko nje kwa dhamana.