Habari za Kitaifa

IG Kanja: Idara ya Polisi inafanyiwa marekebisho kuboresha huduma kwa umma

Na SAMMY WAWERU April 3rd, 2025 Kusoma ni dakika: 1

INSPEKTA Jenerali wa Polisi (IG) Douglas Kanja amehakikishia taifa kuwa serikali inafanya kila iwezalo kufanya mabadiliko kwenye idara ya polisi (NPS), ili kuboresha utoaji huduma kwa umma.

IG Kanja ametoa hakikisho hilo, Alhamisi, Aprili 3, 2025 alipofanya ziara ya ghafla katika kituo cha polisi cha Timau, Kaunti ya Meru.

“Idara ya Polisi inafanyiwa marekebisho ili kuboresha huduma kwa wananchi na kuimarisha usalama nchini,” akasema Bw Kanja.

Kwenye ziara yake Meru, Bw Kanja alikuwa ameandamana na wakuu kadha wa NPS, akiwemo naibu wake kutoka kitengo cha AP, Gilbert Masengeli.