Kamati ya kupiga msasa yapitisha mawaziri wote 20 wateule
KAMATI ya Bunge ya kupiga msasa imepitisha mawaziri wote wateule waliofika mbele yao kuelezea ufaafu wao katika nyadhifa walizoteuliwa.
Kamati hiyo iliyoongozwa na Spika Moses Wetang’ula imepitisha mawaziri hao wateule waliojumuisha John Mbadi (Fedha), Kithure Kindiki (Usalama wa Ndani), Kipchumba Murkomen (Michezo), Hassan Joho (Madini), Davis Chirchir (Barabara), Soipan Tuya (Ulinzi) na Opiyo Wandayi (Kawi) miongoni mwa wengine.
Hiyo inamaanisha kwamba ripoti ya msasa itawasilishwa kwenye Bunge lote, kujadiliwa na kupigiwa kura kwa mara ya mwisho kabla ya kuapishwa na Rais William Ruto.
Kupitishwa kwa mawaziri hao wateule kunajiri wakati kukiwa na pingamizi nyingi kuhusu baadhi ya wateule hao, haswa ule wa Kindiki, Joho, Murkomen na Wandayi huku makundi ya wanaharakati wakiwasilisha kesi kortini Jumanne.