Mwili wa Mkenya kusalia Everest badala ya kuzikwa
NA MWANDISHI WETU
MWILI wa mkweaji Joshua Cheruiyot Kirui aliyega dunia akikaribia kufika katika kilele cha Mlima Everest utasalia katika huo mlima mrefu zaidi duniani baada ya familia kushauriana na kuafikia uamuzi huo.
Familia ya mwenzazake iliweka kwenye mizani changamoto zote ikaona heri mwili usalie huko Everest nchini Nepal.
Soma Pia: Mkenya Cheruiyot Kirui alielewa kibarua cha kuukwea Mlima Everest
Kirui alitoweka Jumatamo wiki jana akikwea Mlima Everest, hali iliyovunja ndoto yake ya kufika katika kilele cha mlima huo wa urefu wa mita 8,848.
“Cheruiyot alitumbukia kwa shimo la theluji mita 48 kabla ya kufikia kilele cha mlima (mita 8,848) na kuuopoa mwili kutoka hapo juu ni hatari kwa waokoaji, familia haitaki kuweka maisha ya mtu yeyote hatarini. Cheruiyot alipenda milima, nayo milima ilijibu kwa kumpenda. Tunafarijika tukifahamu kwamba analala mahali ambapo alipenda zaidi,” taarifa hiyo ya familia ilisema Jumatano.