Spika Wetangula aahirisha kikao cha bunge cha asubuhi, akiahidi kutoa tangazo muhimu
SPIKA wa Bunge la Kitaifa Moses Wetang’ula ameahirisha kikao cha asubuhi cha Bunge la Kitaifa cha Jumatano, Oktoba 15, 2025.
Kwenye hotuba fupi alipoongoza kikao cha asubuhi cha bunge hilo, saa tatu na dakika 59, Bw Weng’ula alitangaza kuwa bunge hilo litafanya kikao baadaye saa nane na nusu alasiri ambapo atatoa tangazo muhimu.
“Nikitumia mamlaka yangu kwa mujibu wa Sheria ya Bunge nambari 1, ninaahirisha kikao hiki. Kikao kitarejelewa saa nane na nusu leo hii (Jumatano) ambapo nitatoa tangazo muhimu kwa wabunge,” Bw Wetang’ula akasema.
Spika huyo alisema hayo baada ya uvumi kutanda nchini haswa mitandaoni kuanzia alfajiri Jumatano kwamba Waziri Mkuu wa zamani, Bw Raila Odinga amefariki nchini India ambako alipelekwa kupokea matibabu.
Inatarajiwa Spika Wetang’ula atatoa tangazo hilo rasmi kwa wabunge baada ya familia ya Bw Odinga na Rais William Ruto kuthibitisha bahari hizo.