Habari za Kitaifa

Waziri Murkomen azindua sera mpya kulinda polisi

Na GEOFFREY ONDIEKI July 18th, 2025 Kusoma ni dakika: 1

WAZIRI wa Usalama wa Ndani, Kipchumba Murkomen, ameanzisha sera mpya inayolenga kuwalinda maafisa wa polisi dhidi ya lawama zisizo na msingi kuhusu matumizi ya nguvu na silaha.

Kupitia agizo hilo la sera alilotangaza rasmi jana, Murkomen amesema polisi sasa watakuwa na miongozo iliyo wazi na ya kisheria kuhusu wakati na jinsi wanavyoweza kutumia nguvu au silaha wanapotekeleza majukumu yao.

“Kwa sasa kuna sera ya maandishi yenye saini yangu, ambayo wananchi wanaweza kutumia kuniwajibisha.

Lakini pia inalinda haki na mazingira ya kazi ya maafisa wetu wa usalama,” alisema Murkomen akiwa Samburu.

Sera hiyo inasisitiza kuwa polisi wanaruhusiwa kutumia nguvu tu katika hali za kujilinda au kuwalinda wengine dhidi ya hatari ya karibu ya kifo au majeraha makubwa. Aidha, wanapaswa kutumia njia zisizo za vurugu kwanza.

Murkomen pia alitangaza kuwa maafisa watakaohusika katika matumizi ya nguvu watapewa ushauri nasaha pamoja na huduma za kisheria kupitia usaidizi wa Mwanasheria Mkuu.Kwa mara ya kwanza, uchunguzi wa visa vya matumizi ya nguvu utafanywa na maafisa waliobobea, kwa haraka na kwa njia huru, kupitia usimamizi wa Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI)