Afungwa kwa kumpulizia kemikali mwanamume 'fisi'
MASHIRIKA Na PETER MBURU
MWANAMKE ambaye alimvamia mwanamume barabarani na kumpulizia kemikali kwa kuwa aliyaangalia matiti yake alihukumiwa kifungo cha miezi 16 gerezani na mahakama moja ya Uingereza.
Bi Hollie Baker wa miaka 29 alieleza korti kuwa hali ya Bw Lee Pearson kuangalia mwili wake ilimfanya kuhisi vibaya, na kuwa mwanamume huyo alikuwa amesimama karibu naye sana walipokuwa wakizungumza barabarani.
“Nilimwambia asonge nyuma mara nyingi sana. Alikuwa akiangalia matiti yangu sana. Nilimrusha kando na kumwambia aniondokee,” Hollie akaeleza korti.
Wawili hao walikuwa wamejuana kwa mwaka, lakini kisa hicho dhidi ya Lee wa miaka 42 kimebadili mkondo wa uhusiano wao. Almchoma kwa kifaa ya kupiga kwa umeme (shock) mgongoni.
Vifaa vya Taser (ambavyo hutumika kumpiga mtu shock) vimepigwa marufuku kwa matumizi ya umma kwani huwa vinatoa nguvu nyingi sana.
Alieleza korti kuwa alikuwa kifaa hicho ili awe akijikinga.
Lakini mwanamume huyo alieleza korti kuwa hakuwa akitazama matiti ya mwanamke huyo. “Alidhani kuwa ulikuwa mchezo lakini nilihisi kama aliyedungwa kisu- ilinitisha sana,” akaeleza korti.
Upande wa mashtaka ulieleza korti kuwa Hollie alikuwa amenunua kifaa kipya na hivyo aliamua kukijaribu dhidi ya mtu. Korti iliishia kumtupa gerezani mwanamke huyo kwa miezi 16.