Aliyejitetea alinajisi mtoto wa miaka 3 akidhani ni mkewe atupwa jela miaka 125
MASHIRIKA Na PETER MBURU
MWANAMUME kutoka Virginia, Marekani ambaye alieleza polisi kuwa alimnajisi mtoto wa miaka mitatu kimakosa akidhani ni mkewe amefungwa miaka 125 jela.
Jaji wa mahakama ya Mercer Circuit Derek Swope alimfunga Henry Vincent Bennett wa miaka 27 vifungo vya kati ya miaka 25 na 100 kwa makosa mawili aliyoshtakiwa nayo, akisema mtoto huyo huenda akaathirika maisha yake yote.
Hata hivyo, baada ya miaka 50 anaweza kuachiliwa kwa kuhurumiwa, korti ikasema.
Mahakama hiyo ilimpata mshukiwa na makosa Desemba, kabla ya kumhukumu Jumanne, baada ya kurudia mara kwa mara kuwa alidhani mtoto huyo alikuwa mkewe mwenye umri wa miaka 24.
Viongozi wa mashtaka walieleza korti Bennett alifahamisha polisi kuwa mara mbili alimnajisi mtoto huyo alipopanda katika kitanda chake, akidhani ni mkewe.
Mawakili wake, hata hivyo, walisema mteja wao alilazimishwa kusema maneno aliyoambia polisi.
Jaji Swope alisema Bennett atasalia gerezani miaka yote aliyo na uwezo wa kushiriki ngono.
Alikamatwa kwa mara ya kwanza Februari 2018, wakati mtoto huyo alifahamisha familia yake na maafisa wa watoto kuwa alikuwa amedhulumiwa.
Bennett alikiri kwa polisi mara mbili kuwa alimdhulumu kingono mara mbili, ikiwemo ile ya mdomo. Alisema visa hivyo vilifanyika alipokuwa kitandani na mkewe bafuni.
Vilevile, alisema lichanganywa na mtoto huyo wa kilo 13 na mkewe wa kilo 81 (uzito wa mwili) mar azote mbili.
Lakini wakati fulani katika kesi hiyo, Bennett alidai polisi walimlazimisha kukiri hivyo.
Mwanamume huyo alikamatwa pamoja na mkewe April Bennett wakati tu mtoto huyo aliripoti kudhulumiwa, lakini mkewe akaachiliwa baadaye.