• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 10:08 PM
Aliyepandikiziwa figo ya nguruwe aruhusiwa kwenda nyumbani

Aliyepandikiziwa figo ya nguruwe aruhusiwa kwenda nyumbani

WASHINGTON DC, AMERIKA

NA MASHIRIKA

MWANAUME wa kwanza kupandikizwa figo iliyobadilishwa vinasaba kutoka kwa nguruwe aliruhusiwa kwenda nyumbani na Hospitali Kuu ya Massachusetts (MGH).

Richard Slayman, 62, aliruhusiwa kwenda nyumbani, baada ya upasuaji wa dharura wa upandikizaji wa kiungo hicho kutoka kwa nguruwe kufanikiwa.

Fanikio la upasuaji huo limesifiwa na wanasayansi ikiwa ni hatua ya kihistoria katika uwanja wa upandikizaji. Siku za nyuma, upandikizaji wa viungo hivyo kutoka kwa nguruwe vilikosa kufanikiwa.

Taarifa kutoka kwa Hospitali Kuu ya Massachusetts, ilisema Bw Slayman, alikuwa akipambana na ugonjwa wa figo, na alihitaji kupandikizwa kiungo hicho ili kuokoa maisha yake.

Madaktari wake walifanikiwa kupandikiza figo hiyo katika upasuaji uliofanyika kwa saa nne Machi 16, 2024.

Wakidhibitisha fanikio hilo, walisema figo hiyo iliyowekewa Bw Slayman sasa inafanya kazi vizuri na kwamba hahitaji kusafishwa damu mara kwa mara (dialysis).

Uamuzi wa madaktari hao kumruhusu Bw Slayman kuondoka hospitalini kulimpa furaha huku akiwashukuru kwa kumhudumia.

“Wakati huu, ninapoondoka hospitali nikiwa sina deni la afya ambalo limekuwa ni la muda mrefu. Nilitamani kuwa hivi kwa miaka mingi iliyopita,” alisema Bw Slayman.

“Leo ni mwanzo mpya sio kwangu tuu, bali kwao pia,” aliongeza Bw Slayman.

Mkuu wa madaktari kwenye muungano wa viungo katika hospitali hiyo, Bw David Klassen, alisema upasuaji huo wa kutumia viungo vya wanyama hadi kwa binadamu tumaini kubwa miongoni mwa wagonjwa wanaokabiliwa na ugonjwa huo.

“Ingawa kazi kubwa imesalia na inahitajika kufanywa. Nadhani kuna uwezo wa kufaidi idadi kubwa ya wagonjwa. lilikuwa ni swali kuu miongoni mwa madakatari kwenye nyanja hii,” alisema Daktari Klassen.

Hospitali hiyo ilisema Bw Slayman ataendelea kutumia dawa kadhaa za kinga ya mwili, na kufuatiliwa kwa karibu na vipimo vya damu na mkojo mara tatu kwa wiki, na pia kwa ziara za daktari mara mbili kwa wiki.

Madaktari wake wamemuonya Bw Slayman kurudi kazini. Wakisema anahitajika kupumzika kwa muda wa wiki sita. Ili kuchukua tahadhari ya kuepuka maambukizi kwa sababu ya dawa zinazokandamiza mfumo wake wa kinga.

Mkurungezi mkuu wa Idara ya upandikizaji wa figo Bw Leonardo Riella, alitaja kuwepo kwa changamoto katika upandikizaji wa viungo vyovyote vya wanyama kwa binadamu.

“Tunataka wagonjwa warudi kwenye hali zao za kawaida na kufanya mambo yanayofurahia, ili kuboresha ubora wa maisha yao,” alisema Dkt Riella.

  • Tags

You can share this post!

Gereza laeleza kwa nini limemtenga Mackenzie na wafungwa...

Ruto aanza kupigia debe Raila apate kiti cha AUC

T L