Kimataifa

Apple yapunguza idadi ya simu kwa kila mteja corona ikichacha

March 21st, 2020 Kusoma ni dakika: 1

MASHIRIKA na MARY WANGARI

CALIFORNIA, AMERIKA

KAMPUNI ya Apple imepunguza idadi ya simu za iPhones ambazo mtu anaweza kununua mtandaoni.

Kulingana na ripoti mpya, mauzo ya vituo vya mitandaoni vya Apple iPhones na bidhaa nyinginezo za Apple kama vile MacBook na iPad Pro, yamepunguzwa huku mkurupuko wa virusi vya corona ukitatiza usambazaji.

Kampuni ya Apple bado haijafikia upeo wa ununuzi wa bidhaa zake.

Kulingana na vyombo vya habari nchini humo, wateja wataweza tu kununua bidhaa mbili za kila muundo wa iPhone kutoka kwa kituo cha Apple mtandaoni wiki hii.

Hii inamaanisha kwamba wateja wanaweza wakanunua zaidi ya iPhones mbili mradi ziwe za muundo tofauti.

Kwa mfano, endapo mtu anataka kununua simu tatu za iPhone 11, hawezi kuruhusiwa lakini anaweza kununua iPhone 11 Pro na iPhone 1 mbili.

Ununuzi huo umeruhusiwa kwa aina mpya ya miundo ya iPhone za Apple – iPhone 8, iPhone 8 Plus, iPhone XR, iPhone 11, iPhone 11 Pro na iPhone 11 Max. Ununuzi wa iPad Pro na MacBooks pia umedhibitiwa.

Tovuti ya Apple inaonyesha kwamba katika mataifa mengi, kuna kiwango fulani cha bidhaa ambazo Apple inaweza kununua.

Unapodurusu tovuti ya Apple, utaona kuna menu inayodhibiti idadi ya bidhaa zinazoongezwa kwenye kapu.

Mauzo ya Apple hatimaye yalidhibitiwa na Apple mnamo 2007.

Nchini China na maeneo ya Hong Kong na Taiwan na taifa la Singapore, ujumbe huu hujitokeza kwenye orodha ya iPhone katika tovuti.

Ujumbe huu huwafahamisha wateja kwamba ununuzi utadhibitiwa kwa vifaa viwili kwa kila uagiziaji bidhaa.

Hata hivyo, hakuna masharti kama hayo katika tovuti za biashara kimtandao kama vile Amazon.

Apple ilitangaza Machi kwamba itafunga vituo vyote nje ya China hadi notisi nyingine itakapotolewa kutokana na mkurupuko wa virusi vya corona.

Maadamu ulimwengu unapambana na ndwele hilo, uamuzi umefanywa wa kufunga vituo vyote katika mataifa mengine ikihitajika.