Baadhi ya raia Algeria wakasirishwa na hatua ya Abdelaziz Bouteflika
Na AFP
ALGIERS, ALGERIA
RAIA wa Algeria aghalabu wasiopenda kiongozi wa kutaka kudumu mamlakani Jumatatu walipuuzilia vikali matamshi ya Rais Abdelaziz Bouteflika kuwa akichaguliwa tena kwa muhula wa tano sasa atakubali kustaafu, wakiapa kuandamana kumsukuma kujiuzulu.
Rais huyo, ambaye amekuwa akiugua kutoka 2013 kupitia barua iliyosomwa katika runinga ya serikali Jumapili, hata hivyo alisema hatakuwa katika orodha ya wagombea Urais, baada ya “kusikia kilio cha raia.”
“Naahidi kutogombea katika uchaguzi huo ambao nitahakikisha kuwa naridhiwa uongozi kwa njia nzuri na kwa utulivu, uhuru na uwazi,” barua ya Rais huyo ikasema.
“Nilisikia kilio kutoka kwa nyoyo za waandamanaji, hasa maelfu ya vijana ambao walizua maswali kuhusu mustakabali wa taifa letu,” barua hiyo ikasema.
Ujumbe huo ulifuatia hatua yake ya mbeleni ambapo alikuwa amesema atagombea Urais kwenye uchaguzi wa Aprili 18, kupitia meneja wake wa kampeni Abdelghani Zaalane, ambayo ilivutia maandamano mengi Jiji kuu la Algiers na miji mingine.
Raia wan chi hiyo walikuwa wakiandamana hadi Jumatatu, wakipinga ahadi ya Rais Bouteflika kuwa wakimchagua kwa mara ya tano atastaafu kwa Amani na kusema kuwa anadhani kuwa wao “ni wajinga.”
“Sisi kama watu milioni 42 tulimkataa Bouteflika, anadhani sisi ni wajinga,” akasema kijana wa miaka 22 kwa jina Karim.
Raia wanapinga hatua ya Rais huyo kutaka mamlaka hadi kifo, wakisema anataka wamwone kama mwokozi wao wa pekee.
Imekusanywa na Peter Mburu