Kimataifa

Burkina Faso yakemea Nigeria kutumia anga yake ilipotuma ndege kuzima mapinduzi Benin

Na REUTERS December 10th, 2025 Kusoma ni dakika: 1

ABUJA, NIGERIA

MATAIFA yanayopatikana ukanda wa eneo la Sahel yameshutumu Nigeria kwa kukiuka kanuni zao za angani.

Nchi hizo zinasema ndege moja ya kivita ya Nigeria ilitua Burkina Faso mnamo Jumatatu bila idhini.

Nigeria haijazungumzia kisa hicho japo imetuma ndege na wanajeshi wake kuzima mapinduzi kule Benin ambayo ni jirani ya Burkina Faso.

Malalamishi hayo yaliibua taharuki inayoendelea kupanda katika mataifa ya ukanda wa Sahel na Muungano wa Kiuchumi wa Nchi za Magharibi mwa Afrika (ECOWAS).

Uhasama huo pia umeshirikisha Nigeria ambayo ina jeshi kubwa Magharibi mwa Afrika.

Mali, Burkina Faso na Niger ziliunda Sahel baada ya kujiondoa Ecowas.

Nchi za Sahel zilisema kuwa ndege ya Nigeria iliyokuwa imewabeba rubani wawili na abiria tisa ilikuwa imepaa anga ya Burkina Faso bila idhini ya nchi hiyo.

Zilisema ndege hiyo ilitua kwenye jiji la Bobo Diaoulasso kwa njia ya dharura. Nchi za Sahel zilisema kuwa zipo ange na hazitaruhusu ndege yoyote kupaa kwenye anga zao.

Mali, Burkina Faso na Niger zilibuni muungano wao wa Sahel baada ya mapinduzi kufanyika.

Walichukua hatua hiyo kuyazuia mataifa ya kigeni kuingilia shughuli zao pamoja na kuepuka vikwazo vya kiuchumi vya Ecowas.