Kimataifa

CORONA: Iran yakataa msaada wa Amerika

March 23rd, 2020 Kusoma ni dakika: 1

NA AFP

KIONGOZI wa kidini nchini Iran, Ayatollah Khamenei, amepuuza taarifa ya Amerika kuwa ina nia ya kusaidia Iran kukabiliana na virusi vya corona.

Badala yake, Khamenei amesema huenda Amerika ndiyo iliyosababisha virusi hivyo.

Khamenei alishikilia kwamba Iran haihitaji msaada wa Rais Donald Trump anayosema ina nia ya kupeleleza na kupata habari muhimu kuhusu nchi hiyo.

“Taarifa ya Amerika haina mashiko hata kidogo. Wanashukiwa wameunda virusi vya corona na sasa wanataka kutumia ujanja wao kudanganya Iran. Kwa nini wanasisitiza kwamba tutume ombi watusaidie na hatuhitaji msaada wao?” akasema Khamenei.

Iran imeripoti zaidi ya watu 20,600.

walioambukizwa virusi vya corona huku wengine zaidi ya 1, 500 wakiaga dunia baada ya taifa hilo kuathirika.