Ebola yazuka upya DRC
NA MASHIRIKA
Kinshasa, DRC
Nchi ya Jmahuri ya Kidemokrasia ya Congo ilitangaza kuibuka tena kwa ugonjwa wa Ebola kwa mara ya kumi na moja.
Waziri wa Afya wa nchi hiyo Eteni Longondo alisema kwamba ugonjwa huo umeibuka katika mji wa Mbandana, kusini magharibi mwa Kinshasa.
“Sampuli zilizopimwa katika kituo cha utafiti cha Kinshasa zilionyesha kuwa zilikuwa na virusi vya Ebola,” alisema Eteni.
“Kikosi cha kukabilliana na Ebola kiko tayari mikoani na kingine kitatumwa kutoka Kinshasa ili kuimarisha vita dhidi ya Ebola. Siku chache zilizopita mamlaka ya mji wa Mbandaka iliripoti vifo vinne.
Katibu wa Shirika la Afya Duniani Tedros Addhamon Ghebreyesus alisema kwa mtandao wa Twitter kwamba kuna visa sita vya Ebola idadi hiyo ikihusisha watu wanne waliofariki.
Tangazo hilo la maambukizi mapya linajiri miaka miwili baada ya DRC kutanganza kuisha kwa maambuziki ya janga la kumi la Ebola lilokithiri kaskazini mwa nchi hiyo mwaka wa 2018.
Janga hilo liliacha watu 3,000 wakipatwa na ugonjwa huo huku wengine 2000 wakiaga dunia.