Kimataifa

Foleni ya kilomita 12 wanandoa wakisaka talaka za haraka

May 28th, 2019 Kusoma ni dakika: 1

MASHIRIKA Na PETER MBURU

MAELFU ya raia wa Ireland walijitokeza nje ya mahakama za nchi hiyo Jumatatu kushiriki zoezi la kupiga kura ili kupunguza muda ambao talaka zinaweza kukubaliwa, wakipiga foleni za hadi kilomita 12.

Maelfu ya wanandoa ambao wanataka talaka zao kukubaliwa kortini ndio waliongoza zoezi hilo, eneo la Dublin foleni ya urefu wa kilomita 12 ya wanandoa ikipigwa nje ya mahakama, wakisubiri zifunguliwe.

Wanandoa hao walijitokeza kwa wingi ili kufanya uamuzi ambao utafanya talaka zao kukubaliwa kwa usawa na haraka, japo foleni zilikuwa ndefu sana.

Asilimia 82 ya raia walipiga kura kupunguza muda ambao talaka zinaweza kukubaliwa kutoka miama minne hadi miwili, na pia kuruhusu talaka zinazofanyiwa nje ya mipaka ya nchi hiyo.

Tofauti baina ya wanandoa zilikuwa zikishuhugiwa hadi katika foleni hizo, wengi wakibishana na kuzomeana mbele ya watu, ishara hasa ya jinsi minyororo ya ndoa imewaweka jela za roho.

Hata hivyo, kuna hofu kuwa watu wengi nchini humo wanaoana kisha kutalikiana, kwani wengine wanadhani ni jambo la kufurahiwa sasa.