Kimataifa

Gen-Z Nepal wampa shinikizo waziri mkuu mpya, wataka akamate wafisadi

Na REUTERS September 24th, 2025 Kusoma ni dakika: 1

KATHMANDU, NEPALA

WAZIRI Mkuu mpya wa Nepal, Sushila Karki hana muda wa kupumua huku vijana waliomng’oa mtangulizi wake wakimtaka atimize matakwa yao kisha uchaguzi uandaliwe ndani ya miezi sita.

Gen-Z sasa wanamtaka Karki, 73, ahakikishe kuwa viongozi wakuu wa vyama waliohusika na ufisadi wanakamatwa.

Pia wanataka wanasiasa mibabe waondolewe kwenye nyadhifa muhimu na pia uchunguzi ufanywe ili waliohusika na mauaji ya watu 74 wakati wa maandamano ya mwezi huu wanaadhibiwa vikali kisheria.

Japo wanamuunga Karki, baadhi wamemkosoa kwa kuvumilia ufisadi alipohudumu kama jaji mkuu.

Pia hawana subira naye wakimtaka ahakikishe mawaziri ambao walikuwa wakihudumu kwenye serikali iliyopinduliwa pia wanakamatwa.

Nepal inashikilia nambari 107 kati ya 108 kwenye ripoti ya Shirika la Kimataifa la Transparency 2024 kuhusu ufisadi.