Guinea kufanya uchaguzi mkuu wiki hii
JUMLA ya watu milioni 6.8 Guinea wanatarajiwa kujitokeza siku ya Jumapili Desemba 28, 2025 kuchagua rais mpya.
Wagombea wa kiti hicho ambao ni tisa akiwemo kiongozi wa kijeshi nchini humo Jenerali Mamady Doumbouya, wamefanya mikutano yao ya mwisho ya kampeni za kisiasa Desemba 24, 2025 kabla ya uchaguzi mkuu mwishoni mwa juma.
Licha ya ahadi yake ya awali ya kurudisha mamlaka kwa raia alipochukua hatamu mwaka 2021, Doumbouya anagombea urais katika uchaguzi ambao upinzani wote mkuu umezuiwa.
Tangu uhuru wake mwaka 1958, Guinea imekuwa na historia tata ya utawala wa kijeshi na wa kimabavu.