Jeshi la Israeli lawauwa watu 10 kusini mwa Syria
WATU 10 wameuawa Novemba 28, 2025 kwenye operesheni ya wanajeshi wa Israeli iliyofanyika kusini mwa Syria.
Hili likiwa shambulio baya zaidi tangu kuondolewa mamlakani kwa Bashar al-Assad takriban mwaka mmoja uliopita.
Jeshi la Israeli limesema mapambano katika operesheni ya kuwakamata wanamgambo kutoka nchi jirani ya Lebanon katika kijiji cha Beit Jin nchini Syria umesababisha kujeruhiwa kwa wanajeshi wake sita wengine wakiachwa katika hali mahututi.
Jesi la Israeli limesema limewalenga wapiganaji wa Jamaa Islamiya.
Jeshi hilo limesema walengwa wa operesheni hiyo ni wapiganaji wa kundi la itikadi kali la Jamaa Islamiya lililo na makazi yake katika nchi jirani ya Lebanon.
Wanawake na watoto ni miongoni mwa waliouawa.