Kimataifa

Joe Biden kutia saini amri kuu ya ‘kukazia’ wahamiaji

May 31st, 2024 1 min read

NA MASHIRIKA

WASHINGTON, AMERIKA

RAIS wa Amerika Joe Biden anatarajiwa kutia saini amri kuu wiki ijayo kuzuia wahamiaji kuingia nchini humo kupitia mpaka wake na Mexico.

Hatua hiyo, inayoonekana kama ya kuimarisha usalama, inaakisi sera iliyoanzishwa na mpinzani wake mkuu katika uchaguzi ujao, rais wa zamani Donald Trump.

Amri hiyo ya Biden itazima nafasi ya wakimbizi kuomba hifadhi nchini Amerika na kuingia kwa wahamiaji, wengi wao kutoka Mexico.

Biden ambaye anaendesha kampeni ya kutaka achaguliwe tena katika uchaguzi wa urais utakaofanyika Novemba 5, 2024, amechukua hatua hiyo baada ya suala hilo la wahamiaji kuchukuliwa kwa uzito na wapigakura wa umri mdogo.

Trump wa chama cha Republican ndiye mpinzani mkuu wa Biden katika uchaguzi huo.