Kansa imeua wanaume wengi kuliko wanawake – Utafiti
LEONARD ONYANGO Na MASHIRIKA
GLASGOW, Uingereza
WANAUME wanafariki kwa wingi kutokana na maradhi ya kansa ya ngozi ikilinganishwa na wanawake, kulingana na utafiti.
Ripoti ya utafiti iliyowasilishwa katika kongamano la saratani katika eneo la Glasgow, Scotland, ilionyesha kuwa idadi kubwa ya wanaume walifariki kutokana na maradhi ya kansa ya ngozi katika mataifa 33 katika kipindi cha miaka 30 iliyopita, ikilinganishwa na wanawake.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, idadi ya wanawake wanaofariki kutokana na ugonjwa huo imepungua.
Utafiti huo uliangazia mataifa 33 ambayo yamestawi kiuchumi barani Ulaya, Amerika Kaskazini na Asia kwa sababu yana rekodi za kusadikika.
“Utafiti huo ulilenga kutuwezesha kufahamu idadi ya watu wanaofariki kutokana na maradhi ya kansa ya ngozi,” akasema Dorothy Yang, an up-to-date analysis of recent melanoma mortality rates across the world to try to understand these patterns, and whether new diagnosis, treatment and prevention strategies are having any effect,” said Dr. Dorothy Yang, aliyeongoza kikosi cha watafiti walioandaa ripoti hiyo.
Watafiti hao walibaini kuwa kansa ya ngozi inaweza kugunduliwa mapema kwa kupima damu.
“Vifo vinavyotokana na maradhi ya kansa ya ngozi vinazidi kuongezeka kila mwaka kote duniani.
“Kadhalika, tulibaini kwamba idadi kubwa ya wanaume wanaugua ugonjwa huo kwa sababu hawajikingi kutokana na miale ya jua,” akasema.
Watafiti hao wanapendekeza kufanyika kwa utafiti zaidi ili kubaini ni kwa nini wanaume wako katika hatari zaidi ya kuugua maradhi ya kansa ya ngozi ikilinganishwa na wanawake.
Mataifa ya Australia na Slovenia yanaongoza duniani kwa kuwa na idadi kubwa ya watu wanaofariki kutokana na kansa ya ngozi.
Wanaume wa 5 kati ya 100,000 nchini Australia wanaugua maradhi ya kansa ya ngozi ikilinganishwa na wanawake 2 kati ya 100,000.
Watu 14,000 wanagunduliwa kuwa na maradhi ya kansa nchini Australia kila mwaka.
Mataifa mengine yaliyo na idadi kubwa ya waathiriwa wa kansa ya ngozi ni Slovakia na Croatia.
Nchini Uingereza, wanaume 3 kati ya 100,000 wanaugua ugonjwa wa kansa ya ngozi ikilinganishwa na mwanamke 1 kati ya 100,000.
Kati ya mataifa yaliyofanyiwa uchunguzi, Japan na Jamhuri ya Czech yanaongoza kwa kuwa na idadi ndogo zaidi ya watu walio na maradhi ya kansa ya ngozi.