Kimataifa

Kimbunga Eta chasababisha maafa nchini Nicaragua

November 7th, 2020 Kusoma ni dakika: 1

Na AFP

GUATAMALA CITY, Nicaragua

JUMLA ya watu 150 wameuawa au hawajulikani waliko jijini Guatamala kufuatia mkasa wa maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na kimbunga Eta.

Kimbunga hicho kiliathiri pakubwa kijiji kimoja kaskazini mwa nchini kulingana na Rais Alejandro Giammattei.

Idadi hiyo ya maafa ni kando zaidi ya watu 18 waliofariki kwingineko katika Amerika ya Kati tangu kimbunga Eta kilipoanza kusababisha maparomoko ya ardhi nchini Nicaragua, Jumanne.

Giammatttei alisema kikosi cha wanajeshi kiliwasilisha katika kijiji hicho kwa jina Queja kuanza shughuli ya uokoaji, huku kukiwa na hofu kwamba idadi kubwa ya watu walikuwa wameuawa.

Ripoti za awali zinasema kuwa “nyumba 150 zimefunikwa na watu 100 wameuawa,” akasema.

Giammattei aliongeza kuwa mkasa mwingine wa maporomoko wa ardhi ulitokea katika eneo la Huebuetenango liliko karibu na mpaka wa nchi hiyo na Mexico ambapo watu 10 walifariki.

“Tulifanyaka makadirio kati ya waliofariki na wale ambao haijulikani waliko na tukapata kwamba ni watu 150 wamekufa,” Rais Giammmattei akasema.

Kufikia Alhamisi ni watu 50 walikuwa wamefariki.