Kimataifa

Korti yaondoa sheria muhimu iliyowekwa na Trump

June 16th, 2024 Kusoma ni dakika: 1

NA MASHIRIKA

WASHINGTON DC, AMERIKA

MAHAKAMA ya Kilele nchini Amerika imeondoa marufuku iliyowekewa silaha maalum zinazowezesha bunduki kufyatua risasi kwa kasi.

Hatua hiyo imetupilia mbali sheria nyingine ya kudhibiti matumizi ya bunduki nchini humo.

Sheria hiyo ilianzishwa 2019 na serikali ya Rais mstaafu Donald Trump baada ya silaha hizo kutumika katika mauaji ya ufyatulianaji risasi yaliyotekelezwa 2017 ambapo watu 58 waliuawa katika tamasha za mziki jijini Las Vegas.

“Uamuzi wa leo umetupilia mbali sheria muhimu ya kudhibiti bunduki. Waamerika hawafai kuishi kwa hofu kuhusu maangamizi ya watu,” alisema Rais Joe Biden kuhusu uamuzi wa Korti ya Kilele.