Kimataifa

Mwanamke aiomba korti imlazimishe mumewe amtaliki

October 19th, 2018 Kusoma ni dakika: 1

MASHIRIKA NA GEOFFREY ANENE

MWNAMKE mmoja jumaa ameomba mahakama nchini India itamatishe ndoa yake ya miaka 16 kwa sababu mume wake ameshindwa kumlisha yeye pamoja na watoto wao wanne.

Kwa mujibu wa gazeti la Sundiata Post, mke huyo Hafsat Zakaria pia alieleza mahakama hiyo ya Sharia mjini Minna kwamba mume wake Umar Aliyu hatoi fedha za kufanya mahali wanakoishi paonekana nyumbani.

“Mume wangu hatimizi majukumu yake ya kuhakikisha tuna chakula.

“Pia ameshindwa kutoa fedha za kufanya mahali tunaishi paonekane nyumbani na za kulea watoto wetu wanne.

“Hii ndio sababu nalilia korti hii ya heshima kutamatisha ndoa yetu,” alisema.

Akijitetea, Aliyu, hata hivyo, alipinga madai hayo akisema alijikaza kisabuni kila mara kuona familia yake inaishi vyema.

Aliambia mahakama kwamba mke wake anatafuta vijisababu tu ili kuvunja ndoa yao. Aliyu alisema bado anapenda mke wake na alitaka waendelee kuishi pamoja kama bwana na bibi.

Akitoa hukumu yake, Jaji Mohammed Habib alishauri wanandoa hao wakumbatie amani akisema ndoa inahitaji utulivu na maelewano.

Habib alisema korti hiyo itawapa fursa watatue tofauti zao kwa amani. Aliahirisha kesi hiyo hadi Novemba 1 kusubiri ripoti yao kuhusu suluhu watakayokuwa wamekubaliana.