Nguli wa miereka wa Amerika Hulk Hogan aaga dunia
MPIGANAJI miereka na mtumbuizaji mahiri Hulk Hogan ameaga dunia, habari kutoka vyanzo vya familia vilivyonukuliwa na vyombo vya habari vya Amerika zimeripoti.
Hogan, ambaye alikuwa na umri wa miaka 71 amefariki kutokana na mshtuko wa roho, ripoti zinasema.
Anafahamika zaidi kupitia kipindi cha miereka cha WWE Wrestling ambacho kilivuma katika miaka ya nyuma kikijumuisha watumbuizaji wengine kama vile The Rock, John Cena, Steve Austin, The Undertaker na Ray Mysterio.
Rais wa Amerika Donald Trump ni miongoni mwa watu mashuhuri waliotuma risala za rambi rambi kufuatia kifo cha Hogan.
Habari zaidi zinafuata…