Kimataifa

Papa Leo amtawaza kuwa Mtakatifu, mvulana aliyekufa akiwa na umri wa miaka 15

Na MASHIRIKA September 8th, 2025 Kusoma ni dakika: 1

ROMA, Italia

PAPA Leo XIV Jumapili alimtawaza mvulana aliyekufa akiwa na umri wa miaka 15, na mtaalamu wa kompyuta, kuwa Mtakatifu wa kwanza mwenye umri mdogo.

Papa Leo alimtawaza Carlos Acutis, aliyekufa 2006, wakati wa ibada ya wazi katika Kanisa la St Peter’s Square iliyohudhuriwa na maelfu ya watu, wengi wao wakiwa wenye umri mdogo na wanandoa wenye watoto wadogo.

Hatua hiyo ilikipa kizazi kijacho cha Wakatoliki mtu wa kuiga ambaye alitumia teknolojia kueneza mafunzo ya kanisa hilo hadi akapewa jina, “Mshawishi wa Mungu.”

Wakati wa ibada hiyo, yake ya kwanza ya kuwatawaza Watakatifu, Papa Leo pia alitawaza Pier Giorgio Frassati, mtu mashuhuri nchini Italia, na alikufa akiwa na umri mdogo.

Leo alisema wanaume hao wawili walionyesha mfano bora kwa kuishi maisha ya kujitolea huku kutumia talanta zao kutumikia Mungu.

“Hatari kubwa maishani ni kuishi nje ya mpango wa Mungu,” akasema katika mahubiri yake.

“Kutawazwa kwa watawa hawa wapya kunatuwasia sote, haswa wenye umri mdogo, kwamba hatufai kutumia vibaya maisha yetu ila tuyatumie kujenga mifano ya kuigwa,” akaongeza.

Vatican ilisema Makadinali 36, Maskofu 270 na mamia ya mapadre walikuwa wameahidi kushirikiana na Papa Leo katika ibada hiyo kuonyesha kuwa Watakatifu hao wanaungwa mkono na uongozi pamoja na waumini wa kawaida.

Hafla hizo mbili zilikuwa zimeratibiwa kufanyika mapema mwezi huu, lakini zikaahirishwa kufuatia kifo cha Papa Francis mnamo Aprili.