Kimataifa

Papa mpya kujitokeza hadharani wakati wowote sasa

Na BENSON MATHEKA May 8th, 2025 Kusoma ni dakika: 1

MOSHI mweupe ulitoka kwenye paa la Kanisa Sistine Chapel jijini Vatican, Roma jana jioni kutangaza kuchaguliwa kwa kiongozi mpya wa Wakatoliki 1.4 bilioniduniani.

Papa alichaguliwa kumrithi Papa Francis aliyefariki dunia Jumatatu ya Pasaka akiwa na umri wa miaka 88 na kuzikwa siku saba baadaye.

Umati katika Uwanja wa Mtakatifu Petro ulilipuka kwa shangwe huku kengele zikilia kutoka kwenye kanisa kuu la Vatican, kuthibitisha kwamba makadinali 133 waliokuwa wakishiriki uchaguzi  tangu Jumatano walikuwa wamefikia uamuzi wa theluthi mbili kuhusu  mrithi wa Papa Francis.

Jina la papa mpya litatangazwa baada ya taratibu zote kukamilika, ambapo sasa atajitokeza hadharani na kusalimia umati wa waumini.

Habari zaidi kadiri tunavyozipata…