Polisi waanza uchunguzi kuhusu moto uliochoma chuo cha Makerere
Na Daily Monitor
Maafisa wa polisi wa nchi jirani ya Uganda wameazisha uchunguzi kubaini ni nini kilichosababisha kuzuka kwa moto ambao umechoma jengo kuu la chuo kikuu cha Makerere.
Kulingana na habari za polisi moto huo unaaminika kuanza Jumapili usiku kwenye paa huku ukisambaa kwenye jengo zima linalowekwa rekodi za chuo hicho pamoja na idara ya fedha..
“Mali nyingi imeharibiwa. Uchunguzi unaendelea ili kubaini kilisababisha moto huo,” ilisema ripoti ya polisi.
Naibu chanzela wa chuo hicho Profesa Nawangwe alisema kwamba watalijenga tena jumba hilo likae vyenye lilikuwa kitambo kwa wakati mfupi”.
“Nisiku ya kuhuzunisha kwa chuo kikuu cha Makerere Jengo letu la afisi kuu na usimamizi limeteketea huku vitu mingi zikiharibika,”alisema Prefesa Nawangwe kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter.
Mama wa Taifa wa Uganda Jane Museveni ambaye pia ni Waziri wa Elimu alitarajiwa kufika kwenye eneo la tukio.
Tafsiri na Faustine Ngila