Kimataifa
Putin kifua mbele uchaguzi ukinukia
NA MASHIRIKA
MOSCOW, URUSI
KURA ya maoni inaonyesha Rais wa Urusi Vladimir Putin anaweza kushinda uchaguzi wa Machi kwa asilimia 82.
Hii ni kulingana na kura ya maoni iliyofanywa na taasisi ya utafiti ya VCIOM.
Wagombeaji watatu wa upinzani, kulingana na utafiti huo, wana uwezo wa kupata asilimia 5 hadi 6, kila mmoja katika uchaguzi huo.
Kura za maoni za Urusi zinatazamwa kama mbinu muhimu ya serikali kufanya tathmini ya ufanisi wa propaganda za Kremlin.