• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 10:08 PM
Rais wa moja ya taifa thabiti zaidi kidemokrasia Afrika, Namibia, afa kwa saratani

Rais wa moja ya taifa thabiti zaidi kidemokrasia Afrika, Namibia, afa kwa saratani

NA WANDERI KAMAU

RAIS William Ruto, Jumapili aliwaongoza Wakenya kutuma rambirambi kwa watu wa Namibia, kufuatia kifo cha Rais Hage Geingob.

Rais Geingob, 82, alifariki mapema Jumapili katika hospitali ya Lady Pohamba Hospital, katika jiji kuu la taifa hilo, Windhoek, majuma kadhaa baada ya kubainika alikuwa akiugua saratani.

Kwenye ujumbe wake, Rais Ruto alimsifia marehemu kama kiongozi aliyekuwa amejituma kuwaongoza raia wa Namibia kwa kujitolea kwingi.

“Ningependa kutoa rambirambi zangu kwa familia na watu wa Namibia kufuatia kifo cha Rais Geingob. Alikuwa kiongozi aliyeamini katika Afrika yenye umoja, ambapo aliimarisha sauti na mwonekano wa bara hili duniani kote. Namwomba Mungu awape nguvu watu wa Namibia wakati huu mgumu wa maombolezo,”  akasema Rais Ruto kwenye kupitia mtandao wa ‘X’.

Kulingana na taarifa kutoka kwa Kaimu Rais wa Namibia kwa sasa, Nangolo Mbumba (ambaye amekuwa makamu wa rais), marehemu Geingob alifariki akiwa na mkewe na watoto wake.

“Watu wa Namibia wamempoteza mtumishi aliyejitolea kuwahudumia watu, shujaa wa kupigania ukombozi, mtengenezaji mkuu wa katiba yetu na nguzo ya uthabiti wa Namibia,” akasema kiongozi huyo.

Geingob alitangaza mwezi uliopita kwamba alikuwa ashaanza kupata matibabu ya maradhi hayo, baada ya kugundulika alikuwa akiugua kwenye ukaguzi wa kawaida wa hali ya afya mwilini mwake.

Tangazo lake, hata hivyo, halikutoa maelezo zaidi kuhusu maradhi hayo.

Hata hivyo, alisema kwamba angeendelea kutekeleza majukumu yake kawaida kama rais.

Mnamo Februari 2, afisi yake ilitangaza angesafiri nchini Amerka kupata matibabu zaidi.

Geingob alichaguliwa kama rais wa tatu wa taifa hilo mnamo 2014. Hapo awali, alikuwa amehudumu kwa miaka 12 kama Waziri Mkuu.

Kwa muda mrefu, kiongozi huyo amekuwa na matatizo ya kiafya.

Mnamo 2013, alifanyiwa upasuaji wa ubongo. Mwaka uliofuata, alisema alikuwa amepona saratani ya kibovu.

Taifa hilo limepangiwa kuandaa uchaguzi wa urais na bunge Novemba mwaka huu.

Kulingana na katiba yake, Geingob hangewania, kwani alikuwa ashahudumu kwa mihula miwili. 

  • Tags

You can share this post!

Serikali yazinduka baada ya mkasa jijini

MIKIMBIO YA SIASA: Sukari ya Magharibi kiazi moto kwa Ruto

T L