Trump aondolewa katika ukumbi mmojawapo ufyatulianaji risasi ukitokea nje ya White House
Na MASHIRIKA
WASHINGTON D.C., Amerika
RAIS Donald Trump aliondolewa haraka kutoka Ikulu ya White House na walinda usalama baada ya kisa cha ufyatulianaji risasi kutokea nje ya jengo hilo Jumatatu.
Hata hivyo, Rais huyo ambaye alikuwa katika chumba cha mikutano, baadaye alirejea ndani baada ya kuthibitisha kisa hicho.
“Kulikuwa na ufyatulianaji wa risasi nje ya White House na inaonekana hali hiyo imethibitiwa. Ningependa kushukuru maafisa wa usalama kwa kufanya kazi nzuri,” Trump akasema aliporejea.
Shirika la Ujasusi lilisema kwenye taarifa Jumatatu jioni kwamba kisa hicho kilianza pale mwanamume mwenye umri wa miaka 51 alimkaribia afisa wa kitengo hicho hatua chache karibu na jengo la Ikulu.
“Mshukiwa alimwambia afisa kwamba huyo kwamba alikuwa amebeba silaha. Kisha mshukiwa aligeuka na kujaribu kumpiga risasi afisa huyo lakini akamlemea na kumpiga risasi mguuni.
Hata hivyo, maafisa wawili wa usalama baadaye waliwaambia wanahabari kwamba mwanamume huyo hakuwa na silaha yoyote na “inaonekana kuwa alikuwa akili punguani.”
Kisa hicho hata hivyo kulivuruga mkutano wa Trump kwa namna ambayo haijawahi kushuhudiwa.