• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 9:01 PM
Trump sasa ahusishwa moja kwa moja na ponografia

Trump sasa ahusishwa moja kwa moja na ponografia

NA MASHIRIKA

ALBANY, NEW YORK

NYOTA wa kurekodi video za ngono mtandaoni, Stormy Daniels, Jumatano alikiri kwamba walishiriki ngono na Rais wa Zamani wa Amerika Donald Trump mwaka wa 2006.

Daniels alikiri hayo alipofika mbele ya mahakama.

Kwa saa kadhaa Daniels, 45, alitoa maelezo jinsi alivyolipwa ili kutotoa habari kuhusu kitendo kilichofanyika kati yake na Trump.

Aliwaambia majaji kwamba aliingia matatani baada ya mpango huo kuwekwa hadharani mnamo 2018, akisema alitengwa na kunyanyaswa nyumbani kwake.

Mawakili wa Trump walipinga ushahidi huo wakisema kwamba maelezo, kama vile kauli ya Daniels kuwa Trump hakuvaa kondomu, ni ya kudhalilisha.

Hata hivyo, jaji Juan Merchan alikataa ombi hilo lakini alikubali kwamba mwanamke huyo hakutumia maneno fiche kueleza yaliyotokea kati yake na Trump.

Daniels pia alikiri kwamba “anamchukia” Trump na kwamba nia yake ilikuwa ni kufaidika na tukio hilo.

Maelezo yake kwa nini alijitokeza hadharani baada ya miaka saba ya ukimya na kukanusha pia hayakuwa wazi.

Trump, ambaye anagombea urais mwaka huu kupitia chama cha Republican alikana mashtaka ya kughushi rekodi za biashara ili kuficha malipo ya pesa ya kumfanya Daniels asitoe maelezo na kukana kufanya mapenzi naye.

Timu yake ya wanasheria ilipendekeza kuwa Daniels alikuwa akisaka nafasi kwenye “The Apprentice,” kipindi maarufu cha televisheni ambacho kilikuwa kikiongozwa na Trump.

Daniels alithibitisha kuwa alitumai angepata nafasi kwenye kipindi hicho baada ya kukutana kwao.

“Hiyo ilikuwa siku muhimu kwangu. Hata hivyo, sikuwa nikitarajia hayo yangetendeka,” akasema Daniels.

Daniels alisema walishiriki ngono na Trump baada ya rais huyo wa zamani kumwalika kwenye hoteli yake kwenye mashindano ya gofu ya watu mashuhuri huko Lake Tahoe, Nevada.

Alisema Trump alimwambia: “Hii ndiyo njia pekee ya kutoka kwenye ufukara.”

Daniels, ambaye jina lake halisi ni Stephanie Clifford, alisema alishindwa cha kumwambia Trump.

“Sikusema chochote.”

Hata hivyo, baada ya wao kushiriki mapenzi, aliamua kuondoka kwenye hoteli hiyo haraka iwezekanavyo.

Naye Trump aliwaambia waandishi wa habari nje ya mahakama kuwa kesi hiyo itasambaratika tu.

Kesi hiyo itaendelea tena Alhamisi.

Mwanasiasa huyo wa chama cha Republican, ambaye alihudumu kama rais kutoka 2017 hadi 2021, anasema kesi hiyo ni jaribio la kumzuia kuwania kiti cha urasi ili kumuondoa Joe Biden madarakani.

  • Tags

You can share this post!

Ndoto za Mbappe kuzolea PSG taji la Uefa zazimwa

Kaunti yaondoa marufuku ya kutumia fuo baada ya Hidaya...

T L