Kimataifa

Ujerumani yaahidi kuwekeza zaidi Afrika

November 1st, 2018 Kusoma ni dakika: 1

Na BERNARDINE MUTANU

Chansela wa Ujerumani Angela Merkel amekutana na viongozi kutoka Afrika na kuahidi hazina mpya ya maendeleo.

Katika mkutano Jumanne, Bi Merkel alisema hazina hiyo itasaidia katika kukabiliana na kutoendelea miongoni mwa mataifa ya Afrika, hali ambayo imepelekea wengi kutaka kuhama barani.

Jumatatu, Merkel alitangaza kuwa ataondoka katika ulingo wa kisiasa 2021. Merkel katika uongozi wake wa miaka 13 mwaka wa 2015 alifungua mipaka na kuwaruhusu wahamiaji (wengi wakimbizi) kutoka Afrika kuhamia nchini humo.

Baadhi ya viongozi kutoka Afrika waliohudhuria mkutano huo ni Rais Cyril Ramaphosa (Afrika Kusini), Abiy Ahmed (Ethiopia) na Rais Paul Kagame (Rwanda).

Mkutano huo ulilenga kukuza nafasi ya uwekezaji wa Ujerumani barani Afrika kwa lengo la kuunda nafasi za kazi kwa Waafrika.

Ujerumani tayari imeyapunguzia makampuni yake ushuru kwa lengo la kuyavutia kuwekeza barani Afrika.