Kimataifa

Trump amtetea mwanamfalme kuhusu mauaji

Na REUTERS November 20th, 2025 Kusoma ni dakika: 1

RAIS wa Amerika, Donald Trump, amemtetea Mwana Mfalme wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman, kuhusu mauaji ya mwandishi wa habari Jamal Khashoggi yaliyotokea mwaka 2018.

Trump alisisitiza kuwa kiongozi huyo “hakujua chochote” kuhusu mauaji hayo huku akimkaribisha kwa heshima Ikulu ya White House.

Amerika na Saudi Arabia ziliidhinisha makubaliano ya nyuklia kwa matumizi ya kiraia na mauzo ya ndege za kivita aina ya F-35, huku Trump akijaribu kufunika suala la mauaji ya mwandishi huyo wa gazeti la Washington Post.

Trump alimkaripia mwandishi wa habari aliyemuuliza Mwanamfalme kuhusu mauaji hayo akisema swali hilo “linamvunjia heshima” mgeni wake katika ziara yake ya kwanza Marekani tangu mauaji hayo.

Kauli ya Trump inakinzana na tathmini ya kijasusi ya Amerika ya 2021 iliyohitimisha kuwa Mohammed aliagiza operesheni ya kumuua Khashoggi.