Wahamiaji haramu wanaoingia Italia waongezeka
Na MASHIRIKA
ROME, Italia
IDADI ya wahamiaji haramu wanaoingia Italia kupitia bahari imeongezeka huku wengi wakifanikiwa bila msaada wa mabaharia ilivyokuwa ikifanyika awali.
Kulingana na Wizara ya Usalama wa Ndani ya Italia, wahamiaji haramu 16,347 walifika Italia kati ya Agosti 1, 2019, na Julai 31, 2020, kwa kutumia mashua bila kusaidiwa na mabaharia.
Katika kipindi hicho wahamiaji haramu 5,271 waliokolewa baharini mashua zao zilipopigwa na mawimbi.
Wizara hiyo ilisema idadi ya wahamiaji haramu waliofika salama Italia iliongezeka kwa asilimia 149 ikilinganishwa na idadi yao 8,691 mwaka uliotangulia ambapo wengi waliokolewa baharini.