• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 8:57 PM
Wanaume wako katika uwezekano mkubwa kupata maambukizi ya virusi vya Corona – wanasayansi

Wanaume wako katika uwezekano mkubwa kupata maambukizi ya virusi vya Corona – wanasayansi

MASHIRIKA na MARY WANGARI

WUHAN, CHINA

IDADI ya kubwa ya wanaume kushinda wanawake ndio waathirika waliopata maambukizi  ya virusi hatari vya Homa ya China ambavyo asili yake ni Wuhan katika mkoa wa Hubei nchini China.

Hata hivyo, wanasayansi wamegawanyika kuhusu sababu ya jambo hilo.

Kufikia sasa, virusi hivyo vimeua watu zaidi ya 910 na kuwaambukiza zaidi ya watu 40,000 huku visa vingi vikiwa nchini China.

Utafiti wa hivi majuzi uliohusisha wagonjwa katika hospitali ya Chuo Kikuu cha Wuhan unadhihirisha picha mojawapo kuhusu jinsi ugonjwa huo unavyofanya kazi kwa binadamu kufikia sasa.

Watafiti hao walibaini kwamba kuna uwezekano mkubwa zaidi kwa virusi hivyo kuwaathiri wanaume wazee walio na matatizo mengine ya kiafya.

Zaidi ya asilimia 54 ya wagonjwa katika utafiti huo walikuwa wanaume ambapo umri wa jumla wa wagonjwa ulikuwa miaka 56.

Tafiti nyinginezo zimetoa matokeo sawia.

Utafiti wa wagonjwa 99 katika Hospitali ya Wuhan Jinyintan ulionyesha kwamba kwa jumla umri wa wagonjwa ulikuwa miaka 55 na nusu huku wanaume wakiwakilisha asilimia 68 ya visa vyote.

Utafiti wa mwisho wa wagonjwa karibu 1,100 wanaougua Homa ya China ambao bado unasubiri kuchambuliwa, ulitambulisha umri wa jumla kuwa miaka 47 huku wanaume wakiwakilisha asilimia 58 ya visa vyote.

Data hiyo imesababisha baadhi ya watafiti kushuku kwamba wanaume wana sifa fulani za kibayolojia zinazowafanya kuwa na uwezekano zaidi wa kuambukizwa virusi hivyo lakini baadhi ya watafiti hawana uhakika.

Watafiti katika hospitali ya Wuhan Jinyintan walitoa ufafanuzi sawia kuhusu sababu ya wagonjwa wao wengi wanaougua Homa ya China kuwa wanaume wakiashiria kwamba wanawake huenda “wana uwezekano mdogo wa kuathiriwa na maambukizi ya virusi hivyo.”

Huku kukiwa na uhaba wa data thabiti kuhusu virusi hivyo vipya vya Homa ya China, wanasayansi sasa wamegeukia mkurupuko sawia – mkurupuko wa SARS kutoka 2002 hadi 2003 – ili kupata vidokezo.

Ugonjwa wa SARS pia ulikuwa aina ya virusi vinavyoathiri mapafu vilivyoruka kutoka kwa wanyama hadi kwa binadamu katika soko za kuuzia nyama.

Ugonjwa huo unashiriki asilimia 80 ya sifa zake na virusi hatari vya Homa ya China, na sawa na mkurupuko unaoendelea kwa sasa, uliathiri idadi kubwa zaidi ya wanaume kushinda wanawake.

You can share this post!

Wakazi wa mtaa wa Landless walalama kuhusu ongezeko la visa...

Msahau makosa ya Moi, ashauri Raila

adminleo