• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 5:50 AM
Watu 12 wakamatwa kwa kula eneo la wazi mchana wa Ramadhani

Watu 12 wakamatwa kwa kula eneo la wazi mchana wa Ramadhani

NA THE CITIZEN

POLISI katika eneo la Mjini Magharibi visiwani Zanzibar wamewakamata watu 12 kwa kula na kunywa maeneo ya wazi mchana wa mfungo katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Kula maeneo ya hadhara saa za mchana wakati wa mfungo wa Ramadhani kisiwani Zanzibar ni hatia kwa wenyeji na wageni.

Kaimu Kamanda wa polisi katika eneo hilo Abubakar Khamis Ally alisema watu hao walikamatwa baada ya uchunguzi uliochochewa na video iliyosambazwa mitandaoni ikiwaonyesha watu wakila hadharani katika uwanja wa Mnazi Mmoja Square, kinyume na kanuni ya mfungo katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Watu hao walizuiliwa katika kituo cha polisi cha Madema kuhojiwa kabla ya kufikishwa mahakamani kujibu mashtaka.

Miongoni mwa waliokamatwa ni pamoja na Issa Hamad Juma,40, kutoka Kikwajuni, Hamad Hamis Indole,25, wa kutoka Mtwara, Hashimu Bakari Nassoro,35, wa kutoka Kwarara na Selemani Ismail Nalinga,34, wa kutoka Magogoni miongoni mwa wengine.

Mkuu huyo wa polisi, Ally, alionya kuwa polisi wataendelea kuwakamata watu watakaovunja sheria kwa kula hadharini wakati huu wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

  • Tags

You can share this post!

Hofu kuzaana kuongeza kura kutaangusha Mlima Kenya

Mikakati ya kuzima wanafunzi wanaotumia ChatGPT kufanya...

T L