Habari

Moses Kuria asema amejiuzulu serikali ya Ruto

Na MWANDISHI WETU July 8th, 2025 Kusoma ni dakika: 1

MSHAURI wa Rais kuhusu utekelezaji wa miradi ya umma Moses Kuria ametangaza kwamba amejiuzulu serikalini.

Kulingana na chapisho lake katika mtandao wa X, Bw Kuria anasema alikutana leo Jumanne, Julai 8, 2025 na Rais William Ruto na kwamba “amekubali ombi langu la kuondoka serikalini”.

Hakufafanua zaidi kuhusu sababu kamili ya kuondoka serikalini ingawa katika siku za hivi punde amekuwa akitoa matamshi na machapisho yaliyoibua maswali kuhusu msimamo wake kuhusu masuala kama vile uchaguzi mkuu ujao.

Mengi zaidi ni kadiri tunavyoyapokea…