Njanuari! Wakenya wakaza mishipi bei ya kabeji ikipanda baada sherehe
KWA miaka mingi, kabeji imekuwa chakula cha dharura kwa Wakenya pale fedha zinapokuwa chache.Lakini sasa katika sehemu nyingi za Kenya, bei imepanda huku wakulima kaunti ya Nyandarua wakipata faida adimu kutokana na zao hilo.
Mjini Kisumu ambako kabeji moja ilikuwa ikiuzwa kwa Sh40 au Sh50 miezi michache iliyopita, sasa inauzwa kati ya Sh100 na Sh170, kulingana na ukubwa na soko.
Hata katika maduka makubwa ya reja reja, bei iko juu kidogo, baadhi ya maduka yanauza moja kwa Sh129.
Hata hivyo, katika eneo la Kinangop Kusini, Kaunti ya Nyandarua, wakulima wanauza kabichi kwa Sh30 hadi Sh40, bei ambayo wanasema ndio juu zaidi waliyowahi kupata.
Wakulima wanasema uhaba wa mvua, gharama kubwa za uzalishaji na kuachwa kwa zao baada ya hasara ya muda mrefu ndizo sababu zinazoathiri upatikanaji. “Kabeji ni zao linalohitaji kutunzwa sana.