HabariSiasa

PICHA: Nderemo nje ya mahakama baada ya Obado kuachiliwa

October 24th, 2018 Kusoma ni dakika: 1

NA RICHARD MUNGUTI

MAHAKAMA Kuu Jumatano imemwachilia huru Gavana wa Migori Okoth Obado kwa dhamana ya Sh5 milioni pesa taslimu.

Gavana Okoth Obado alipofikishwa mahakamani Milimani Oktoba 24, 2018. Picha/ Richard Munguti

Punde tu baada ya kupewa dhamana, wafuasi wake walijitokeza kucheza na kuimba nyimbo za furaha nje ya mahakama ya Milimani, nairobi.

Bw Obado afunguliwa pingu alizotiwa. Picha/ Richard Munguti

Ulinzi mkali uliwekwa huku maafisa wa polisi wenye vitoa machozi wakishika doria.

Bw Obado ajawa na furaha baada ya mahakama kukubali kumwachilia kwa dhamana. Picha/ Richard Munguti

Hata hivyo, washukiwa wengine wawili walioshtakiwa pamoja Michael Oyamo na Caspal Obiero walinyimwa dhamana.

Bw Obaro huru, lakini Michael Oyamo na Caspal Obiero watazidi kusalia rumande. Picha/ Richard Munguti

Jaji Jessie Lesiit alisema ushahidi dhidi ya Oyamo na Obiero unawalenga katika mauaji ya Sharon Otieno.

Mwanamume huyu alifurahia huku akisoma Biblia kuona gavana wake ameachiliwa huru. Picha/ Richard Munguti

Akimwachilia Bw Obado jaji huyo alisema ushahidi uliowasilishwa na Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma dhidi ya Obado haujamlenga moja kwa moja. Jaji Lesiit alimwamuru Obado asisafiri zaidi ya kilomita 20 kutoka nje ya Migori.

Mfuasi sugu wa Bw Obado adhidhirisha anavyomuenzi. Picha/ Richard Munguti

Pia alimwamuru Obado asivuruge mashahidi na pia awe akipiga ripoti mara moja kwa mwezi kwa.msajili wa mahakama kuu kitengo cha kushughulikia kesi za uhalifu.

Ilikua nderemo na vifijo nje ya mahakama. Picha/ Richard Munguti

Jaji Lesiit pia alimtahadharisha kwamba akikaidi masharti sita aliyopewa dhamana aliyopewa itaondolewa.

Awali ilibidi maafisa wa polisi wafunge milango na kuwazuia wafuasi hao wa Bw Obado kutoingia mahakamani.

Ilikuwa siku ya furaha kotekote. Picha/ Richard Munguti

Wanahabari, mawakili na jamaa za washtakiwa walizuiliwa kuingia ndani ya mahakama uamuzi ulipokuwa unasomwa.

Walioruhusiwa kuingia mahakamani ni mawakili waliowawakilisha washtakiwa na watu wachache na wapeperushaji wa habari wa runinga.

Wafuasi wa Bw Obado walifungiwa nje ya mahakama. Picha/ Richard Munguti

Wafuasi hao walipiga kambi nje ya mahakama kusubiri mawakili wamlipie dhamana ya Sh5milioni pesa tasilimu ndipo atoke seli.