Habari

Raila Odinga Jr: Nitalinda familia Baba

Na WINNIE ONYANDO October 17th, 2025 Kusoma ni dakika: 1

Raila Odinga Junior, mwanawe Marehemu Raila Odinga, amemsifu babake na kuwafanya mamilioni ya Wakenya waliojaa Nyayo Stadium kushangilia.

Nchi inapoingia katika siku yake ya tatu ya maombolezo ya kitaifa, Raila Junior alisema kuwa atasimama na kuitunza familia yao.

“Nakuhakikishia kwamba nitatunza familia yetu …Asante kwa kunipa jina lako

bila kunitwika jukumu la hilo jina,” alisema Raila Junior.

Kwa upande wake, Winnie Odinga, bintiye marehemu alisema kuwa babake aliaga dunia kishujaa.

“Baba hakufa kama ninavyoona wakisambaza mitandaoni. Alikufa kishujaa. Alikufa mikononi mwangu,’ alisema Winnie.

Winnie alieleza kuwa babake aliangua wakati wa matembezi ya asubuhi.

Bw Odinga aliaga dunia Oktoba 15, 2025 ndani ya uwanja wa kituo cha tiba ya Ayurveda, na alikimbizwa Hospitali ya Macho ya Sreedhareeyam Ayurvedic na Kituo cha Utafiti huko Koothattukulam, ambapo alitangazwa kuwa amefariki dunia.