Tanzania yapiga marufuku noti za Kenya
Na VALENTINE OBARA
BENKI Kuu ya Tanzania imepiga marufuku ubadilishanaji wa sarafu za Kenya kwa zile za Tanzania.
Taarifa iliyoandikwa na benki hiyo ya taifa imesema ushauri kutoka kwa Benki Kuu ya Kenya ulikuwa kwamba ubadilishanaji huo usitishwe kama njia mojawapo ya kukabiliana na matapeli.
Hatua hii ya ghafla imetokea siku chache baada ya CBK kuzindua noti mpya, huku noti za sasa za Sh1,000 zikitarajiwa kupigwa marufuku kuanzia Oktoba 1.
Inahofiwa kuna matapeli walioficha noti hizo za Sh1,000 ambao huenda wakajaribu kuzibadilisha kwa sarafu za kigeni ili kuepuka kunaswa kwenye mtego wa serikali watakapoenda kwa benki kuchukua noti mpya.
“Ili kukabiliana na pesa haramu na feki katika Jamhuri ya Kenya, Benki ya Tanzania imeshauriwa kufunga akaunti ya CBK ya kukusanya sarafu mara moja,” taarifa hiyo ikasema.
Hali hii huenda ikaathiri Wakenya walio Tanzania ambao wana sarafu za Kenya, kwani itawabidi kutafuta mbinu ya kupa