• Nairobi
  • Last Updated December 5th, 2023 10:25 PM
Ada za Idd ambazo ‘zimesahaulika’

Ada za Idd ambazo ‘zimesahaulika’

Na MISHI GONGO

KATIKA dini ya Kiislamu kuna sikukuu mbili ambazo huwa na umuhimu mkubwa kwa waumini.

Sikukuu hizo ni Idd-ul-Fitr ambayo husherehekewa baada ya Ramadhan na Idd-ul-Adha ambayo husherehekewa baada ya kumalizika kwa ibada ya Haji.

Ili sherehe hizo kunoga zaidi jamii mbalimbali walitekeleza ada tofauti kujiburudisha japo hazimo vitabuni.

Hata hivyo baadhi ya ada hizo kwa sasa hazifanyiki tena. Miongoni mwa ada zilizosahaulika ni watoto kuadhimisha sikukuu hiyo kwa vigoma.

Watoto wa mtaa mmoja walijikusanya na kutembelea nyumba baada ya nyumba wakiwatumbuiza watu kwa ngoma na nyimbo za utani.

Watoto hao wangevalia vinyago wakitekeleza yanayojuzu ngoma hizo. Wanaotumbuizwa nao waliwatuza watoto hao kwa pesa, mapochopocho, pipi na kadhalika. Kwa sasa ada hiyo haitekelezwi tena.

Pia watoto walizunguka kwa kila nyumba katika mtaa wao kupokea mkono wa Idd.

Kwa kila nyumba watoto walipewa pesa au pipi. Pesa hizo walizitumia kwenda katika maeneo ya burudani kama fuo za bahari au katika bustani.

Ingawa hivyo, kuna ada zingine ambazo bado zinatekelezwa. Ada hizo ni watoto wa kike kuchorwa piko na hinna.

You can share this post!

Mutula Jr aongoza maseneta wa Ukambani kumkaidi Kalonzo

Corona yafichua visiki katika sekta ya matatu vina suluhu

adminleo