• Nairobi
  • Last Updated April 18th, 2024 5:41 PM
IDD-UL-ADHA: Matiang’i atangaza Ijumaa ni sikukuu

IDD-UL-ADHA: Matiang’i atangaza Ijumaa ni sikukuu

Na CHARLES WASONGA

WAZIRI wa Masuala ya Ndani Fred Matiang’i ametangaza Ijumaa, Julai 31, 2020, kuwa siku ya mapumziko.

Kwenye tangazo lililochapishwa kwenye Gazeti Rasmi la Serikali toleo nambari 5277 waziri amesema Ijumaa itakuwa siku ya sherehe ya Kiislamu ya Idd ul-Adha.

“Kwa kuzingatia umuhimu wa imani kama jambo la kuunganisha jamii nchini, na kutambua kuwa dini na utamaduni ni ishara ya utambulisho wa kitaifa, Ijumaa, Julai 31,2020, imetengwa kama siku ya mapumziko kote nchini kuadhimisha sikukuu ya Idd ul-Adha,” akasema Dkt Matiang’i

Amesema kutokana na janga la Covid-19, sherehe zote za Idd-ul-Adha zitaendeshwa kwa kuzingatia kanuni zilizoweka na Baraza la Viongozi wa Madhehebu Mbalimbali na zile za Wizara ya Afya za kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.

Siku Kuu ya Idd-al- Adha ni ya pili miongoni mwa sherehe za Kiislamu ambazo huadhimishwa kukumbuka imani ya Nabii Ibrahimu kwa Mungu iliyodhihirishwa na kujitolea kwake kumtoa mwanawe wa kiume kama kafara.

You can share this post!

Kenya ina PPE za kutosha, asema Kagwe

Nafasi ya Sakaja yajazwa

adminleo