Ukame wa tendo la ndoa huenda kukaleta athari za kiafya, wataalam wabaini
KUKOSA kushiriki mapenzi kwa kipindi kirefu kunasababisha matatizo ya kiafya ikiwemo saratani na magonjwa ya moyo, Watafiti wamebaini.
Watafiti hao, wanasema kuwa kushiriki tendo la ndoa lenye ubora wa juu, kuna manufaa yake kiafya. Kukosa kufanya hivyo, wanaeleza, kuna athari hasi kiafya ambayo huandamana na shinikizo la damu na maumivu mgongoni.
Wanaume wapo pabaya zaidi kwa sababu kukosa kushiriki mahaba pia kunahusishwa na uwezekano wa kupata saratani ya tezi dume.
“Watu hukosa kushiriki ngono kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo shughuli nyingi, kutokuwa na mpenzi au kuamua tu kuchukua mapumziko baada ya uhusiano wa awali kuvunjika pamoja na imani ya kidini,” wanasema watafiti kutoka Chuo Kikuu cha Anglia Ruskin, Cambridge, Uingereza.
Kukosa kushiriki ngono kwa kipindi kirefu pia kuna athari zake hasa ki hisia katika uhusiano.
“Kusononeka, msongo wa mawazo na wasiwasi kunaweza kutokea kutokana na kukosa kushiriki mapenzi mara kwa mara au ukame wa kipindi kirefu. Ngono pia huimarisha kinga mwilini,” wanaongeza watafiti hao.
Wapenzi ambao hawashiriki ngono mara kwa mara huwa hawana mnato imara au dhabiti kati yao. Kushiriki ngono kunasaidia katika kuzalisha homoni zinazofahamika kama oxytocin na endorphins ambazo zinasaidia kuzuia au kudhibiti msongo wa mawazo na matatizo mengine ya kiakili.
Homoni ya oxytocin pia huimarisha mnato wa kiakili na kumbukizi kwa kuwa pia inasaidia katika kuhakikisha mtu anapata usingizi mzuri.
Ngono pia huimarisha mazungumzo kati ya wapenzi ambao hujawa na furaha pamoja kuweka hisia zao kuwa pamoja na dhabiti.
Wataalamu hao hata hivyo wanashauri si lazima wapenzi washiriki ngono kila siku kwa kuwa hata mara moja pekee kwa wiki huwa imetosha.
Baada ya kupita umri wa miaka 20, wapenzi wanastahili kufanya mapenzi angalau zaidi ya mara mbili kwa mwezi ili kuzuia matatizo yanayotokea mtu asiposhiriki ngono.