Badala ya kujitutumua na mazoezi mazito kula vyakula vya kujenga na kuimarisha misuli
Na MARGARET MAINA
KUJENGA misuli ni kitu ambacho wengi wangependa kufanya katika maisha yao. Kuwa na misuli mwilini husaidia pakubwa kufanya mtu hasa kuinua mizigo mizito bila shida yoyote.
Kuwa na misuli pia hufanya mtu kuweza kuwa na mwili ambao hujikinga wenyewe kutokana na magonjwa ya mara kwa mara na pia humwezesha mtu kuwa na mwili wa kuvutia.
Lakini tatizo kuu n ikuwa wengi hawajui mbinu bora ya kujenga misuli na hujitwika na majukumu au shughuli kama unyanyuaji uzani, kuinua vyuma vizito na kufanyisha miili yao mazoezi mazito ili kuwa na misuli thabiti.
Hivi vitendo kimsingi husaidia lakini pia huumiza mwili kama hutatumia vyakula vinavyohitajika kujenga misuli.
Ni muhimu kwa mtu kuelewa vyakula gani vinavyohitajika katika kujenga misuli na pia kujiepusha na vyakula ambavyo vitakuletea mafuta yasiyokuwa na manufaa kwa mwili.
Nyama isiyokuwa na mafuta
Nyama ya kuku isiyokuwa na ngozi wala mifupa husaidia sana kwa kuupatia mwili wako nguvu ili kuendesha shughuli zote zinazohitajika katika mwili wako.
Samaki
Samaki ni muhimu sana hasa ngege yaani tilapia.Ukila samaki unapata asilimia kubwa ya protini na fatty acids ambazo mwili huhitaji kwa wingi, lakini hauwezi kutengeneza usipopata vyakula aina hii.
Protini ya Soy
Haya madini hupatikanamkwa kutenganisha mbegu za soya na hupatia mwili wako kiwango kikuu cha protini.
Protein Shake
Huu ni mchanganyiko wa protini, mafuta na wanga; vitu vinavyouletea mwili nguvu ambazo hukufanya usihisi njaa kwa muda mrefu. Husaidia pakubwa kwa kujenga misuli.
Maharagwe
Maharagwe ni muhimu na njia rahisi ya kupatia mwili protini. Maharagwe kama ya soya, maharagwe meusi na yale ya ‘kidney beans’ yana kiwango kidogo cha mafuta na hupatia mwili wako aina tofauti za wanga, husaidia kuhimili na kudhibiti kiwango cha sukari na kupunguza uhitaji wa sukari kwa mwili wako.
Mboga
Mboga kama mrenda, mchicha, mboga za kunde na nyinginezo huupa mwili kiwango kikubwa cha maji, madini na pia nyuzinyuzi ambazo hujaza kalori ambazo zimepotea kwa mwili wako.
Matunda
Matunda ya na kiwango kikubwa cha virutubisho pamoja na nyuzinyuzi.
Oatmeal
Chakula hiki husaidia mwili wako kupata nyuzinyuzi pamoja na kusaidia kuendesha shughuli za mwili wako.
Hupunguza haraka isiyo ya kawaida ya kusaga chakula; hali ambayo husaidia kuufanya mwili kuhisi kuwa umeshiba kwa muda mrefu. Pia huchangia kupunguza kiwango cha mafuta mwilini.
Maji
Maji ni muhimu zaidi kwa mwili.