FATAKI: Piga nakshi ujuzi wa kubingirisha kamba kabla kuteta!
Na PAULINE ONGAJI
KATIKA enzi hizi inahuzunisha kwamba kuna idadi kubwa ya madume ambao bado wanatawaliwa na dhana potovu kwamba ubora wa ‘kisima’ cha mwanamke hupungua jinsi orodha ya madume wanaopewa burudani inavyozidi kuongezeka.
Nazungumza haya kuambatana na kisa nilichozungumzia miezi kadha iliyopita kuhusu madume wawili waliokuwa wakimkejeli binti fulani ambaye kulingana nao walikuwa washamuonja, na ambaye kwa viwango vyao, sehemu hii ilikuwa ‘imelegea’.
]“Hata sikuwa na raha kwani binti huyo alikuwa ‘mpana’ ajabu! Kisima kilikuwa sawa na mtaro ambapo nikiwa mle ndani nilihisi kana kwamba nimo baharini kiasi cha kuwa singeweza kufikia ukuta,” alisema mmoja wao.
Lakini upumbavu huu hauathiri tu hawa wanaume wawili. Madume wengi hudhani burudani hutegemea na upana na kina cha kisima huku wakipuuza urefu wa kamba inayoteremsha kifaa cha kuteka maji.
Akina kaka huzungumzia umuhimu wa sehemu hii kuwa thabiti na kusahau kuwa wembamba au udhaifu wa uzi sio kosa la tundu la sindano.
Ujuzi
Ikiwa unahisi kwamba hufikii kingo, pia wewe piga nakshi ujuzi wako wa kubingirisha kamba ili ufikie kuta za kisima, au wende zako ukasake kijisima kinachotikiswa na wembamba, vilevile ufupi wa uzi wako.
Unapata kaka analalama ilhali ana kitambi utadhani ni mwanamke anayekaribia kujifungua.
Hajui kwamba sehemu hii pia hupunguza uwezo wa kamba kufika chini ya kisima.
Haya ni baadhi ya mambo ambayo madume wanapaswa kuzingatia kabla ya kuelekezea mabinti lawama.
Kabla ya ulalame kwamba kisima ni kipana au kina chake ni kirefu, je, una uhakika kwamba kamba ya kuteremsha kifaa chako cha kuteka maji ni refu vilivyo? Huenda unajaribu kutumbukiza uzi kwenye kisima kinachostahimili uzito wa kamba ya kusukuma trekta.
Hata wachimba visima watakuambia kwamba kuna aina mbalimbali za visima kuambatana na upana, vile vile kina, na hivyo kama mteka maji unapaswa kuendea kinachoambatana na urefu wa kamba yako.
Sipingi kwamba kisima pia kinapaswa kushughulikiwa kuhakikisha kwamba matofali au mawe yaliyotumika kuunda kuta zake yako thabiti ili kudumisha usafi wa maji, lakini wanaume hawana haki ya kuwasuta kwani baadhi yao wanaojipiga vifua wakiambiwa ukweli hawatoonyesha nyuso zao mbele ya watu.