• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 10:08 PM
FUNGUKA: Kipigo toka kwa mke hunikolezea mahaba!

FUNGUKA: Kipigo toka kwa mke hunikolezea mahaba!

Na PAULINE ONGAJI

DUNCAN ni mmojawapo wa madume ambao nina uhakika mabinti wengi wangependa kuhusishwa naye.

Bwana huyu mwenye umri wa miaka 43 ni mtaalamu wa masuala ya kifedha katika shirika moja, ajira aliyopokea kutokana na jinsi anavyofahamu masuala haya vyema tangu akiwa chuo kikuu.

Ujuzi wake wa kipekee umemfanya kuwa mmojawapo wa wafanyakazi wanaothaminiwa katika shirika analofanyia kazi.

Aidha, ni mmojawapo wa wafanyakazi wanaopokea mishahara mikubwa pale.

Mbali na masuala ya kikazi, bwana huyu ana sifa za kipekee za kimaumbile, suala linalomfanya kuwa kivutio cha mabinti njiani ambapo imekuwa kawaida kukutana na vipusa wakipindua vichwa kila anakopita.

Lakini kabla ya kummezea mate, kama binti unapaswa kufahamu kwamba Duncan ameoa na ana watoto wanne, kwa hivyo tayari ameshachukuliwa.

Sio hilo pekee ambalo kama binti linapaswa kubadilisha mawazo yako iwapo unamtamani kaka huyu.

Bwana huyu ana mbinu moja ya kustaajabisha anayotumia kuzuzua hisia za mahaba.

Duncan hufurahia kichapo cha mwanamke na anasema kwamba hiki ni kichocheo kikuu wakati huu:

“Nafurahia kuchapwa katika uhusiano ndiposa kabla ya kuoa, mojawapo ya vigezo nilivyokuwa nikitumia kusaka wapenzi, ilikuwa uzani. Ili kufuzu kuwa mpenzi wangu wakati huo, basi ilikuwa lazima uwe umenizidi kwa uzani. Hii ilimaanisha kwamba ulikuwa na nguvu za kunipa kichapo nilichokuwa nahitaji wakati huo.

Kichapo hiki kinahusisha mambo mengi. Yaweza kuwa kichapo cha mijeledi, makofi, ngumi na hata mateke.

Wengi wanadhani huu ni wendawazimu lakini kwangu ni jambo linalonisisimua. Ili nifurahie mahaba lazima nipokee kichapo wakati huu, huku mara nyingi nikifurahia makofi na mangumi na mijeledi mgongoni na miguuni, kabla na wakati wa shughuli. Nisipopokea kichapo hiki, basi mahaba hayawezi kufanyika.

Hata hivyo, kichapo hiki sio kila mara ila tu wakati wa mahaba ambapo mwenzangu anaruhusiwa kunichapa.

Hii ni sababu ambayo imenifanya kuhakikisha kwamba kila binti ninayemchumbia amenizidi uzani na awe na nguvu zitakazomwezesha kunicharaza kwa nguvu.

Nikiwa barubaru ilikuwa vigumu kuhifadhi wachumba kwani licha ya wengi wao kunipenda, ilipowadia wakati wa kunichapa walishindwa, jambo ambalo lilisababisha mahusiano yangu mengi kufikia kikomo.

Ilinichukua muda kabla ya kupata mke kwani pindi binti niliyekuwa nikimchumbia alipogundua chocheo langu wakati wa mahaba, basi alitoweka.

Hata kwa mke wangu haikuwa rahisi kwani ilimchukua muda kabla ya kukubali wito wangu.

Kwa sasa amezoea na anafahamu kuwa anapofanya hivyo basi penzi na mahaba yetu yananoga. Isitoshe, ananipenda zaidi na hata yeye ameanza kukumbatia tabia hii ambapo akinigonga kidogo nami pia namgonga.

Lakini kwa kawaida tunapofanya hivi sote huwa waangalifu ili tusisababishiane majeraha mabaya. Hii imekuwa chocheo la kipekee kiasi cha kuwa huu ukiwa mwaka wa 13 tangu tuoane, uhusiano wetu umekuwa ukiimarika kila kuchao.

Wanandoa wanapaswa kufanya chochote kile cha kuleta msisimuko katika ndoa yao; mradi hakiwadhuru kiafya, badala ya kukaa kitako na kushuhudia uhusiano wao ukidorora.”

You can share this post!

SHERIA: Tatizo la ulaghai wa wahubiri katika usajili wa ndoa

KIJIWENI: Watetezi wa usawa, tukimbie wapi tulioambiwa...

adminleo