• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 6:55 PM
Kazi ya uandishi mitandaoni inalipa

Kazi ya uandishi mitandaoni inalipa

Kevin Rotich

[email protected]

Teknolojia ya kisasa imeipa nyanja ya uandishi umaarufu mwingi kutoka kwa vijana ambao wangependa kupata kipato.

Hii imesababisha kuibuka kwa kuenea kwa uandishi wa mitandaoni kama vile blogu na vitabu vya kidijitali ambavyo vimerahisisha jinsi  waandishi wanavyofanya kazi zao.

Lakini, nyanja hii inahitaji uvumilivu mwingi, kujikaza na kukuza ari ya kutaka kufaulu. Aswani Nabwire ni mmoja wao ambaye anajihusisha na kazi ya kuandika vitabu, magazeti, makala, hotuba, blogu na kutasfiri kazi.

Anasema alianza kazi ya kuandika akiwa katika shule ya upili alipokuwa akikariri mashairi hadi mashindano ya kitaifa yaliyofanyika kila mwaka.

“Lakini, wazazi wangu walitaka nifanye udaktri au uuguzi kwani walidai hayo tu ndio kazi zitakazompa kazi siku zinazokuja,” Bi Aswani anasema.

Alipojiunga na Chuo Kikuu cha Nairobi, yeye alifanya kozi ya utangazaji na uanahabari ambayo anasema alikuwa akivizia tangu awe mdogo.

 Ili kuendeleza tajriba yake katika tasnia ya utangazaji, alifungua blogu yake mwaka wa 2012 ili aweze kuandika Makala mbalimbali katika Jamii.

“Nilipohitimu mwaka wa 2013, nilifanya kazi ya mafunzo kabla ya kuajiriwa kwa muda mrefu. Baadae kazi hiyo iliishia,” anasema.

Alifanya kazi katika benki ya Barclays Bank of Kenya (ambayo sasa ni Absa), Medlink Medical Centre, Global Health Concerns, Royal Media Group na pia Nation Media Group.

Kutokana na ukosefu wa kazi mwaka wa 2018, alijiingiza kwenye kikundi cha kuandika katika mtandao kufanyia watu wengine kazi ya uandishi.

“Kwa wakati huo, nilikuwa natengeza wateja kule Marekani na Canada kwa miradi ya uandishi niliyokuwa naandika kwenye mambo tofauti tofauti hasa biashara,” aliongezea.

Kwa wakati huo, alikuwa anapanga kuandika kitabu chake kinachohusu uzazi kwa wanawake.

Hapa Kenya, alikuwa akifanya kazi ya kuhariri miswada kwa makampuni kadha ambapo aliunda jina lake.

Baadae, alibadilisha blogi yake kuwa wavuti ili aweze kuvutia wateja wengi.

“Ilibidi nibadilishe jina la blogi ili livutie wateja na kuonyesha tajriba ya hali ya juu,” anaongezea.

Kwa wakati ule alichapisha kitabu chake. Hapo ndipo wasomaji wengi walitaka awaandikies hadithi zao kutokana na ushapavu wake katika Nyanja ya uandishi.

“Nilianza kuandikia watu kazi zao wakati pale wao walitaka niwaandike kwa kuwa hawakuwa na wakati wa kuandika,” anasema.

Kando, alikuwa akijiusisha na maelezo ya kitaaluma katika majarida na wasifu.

Anasema kiwango cha chini anachoitisha ni Sh1, 000 kwa kila moja lakini huongezeka kulingana na kazi inayofanywa.

“Kila mteja huja na mahitaji tofauti tofauti. Wakati mwingine sisi ndio tunafanya uchunguzi wa kazi za uandishi na pia mahojiano ya moja kwa moja. Tunalipisha kulingana na kazi,” anasema.

Alipoanza, aliwekeza Sh30, 000 kwenye wavuti iliyohitaji picha, video, na vifaa vya kusomea. “Lakini, kuanza kuandika haikunigarimu sana.”

Anaeleza amewaandika kazi watu watatu kwenye maelezo ya biashara. “Kazi ya uandishi na Makala nafanya pekee yangu labda tu kazi iwe nyinyi ndio nitaitisha msaada,” anasema.

Kwa kazi ya uandishi bila mkataba, anasema, ameajiri mhariri ambaye humsaidia kulingana na kazi na mkataba.

Alipoaanza alikuwa na idadi ya wateja watatu kwa mwezi lakini sasa huwa 12, kulingana na miezi.

“Siwezi kuchukua kazi nyinyi kwa wakati mmoja kwani kiwango cha ubora utashuka na kufanya wateja kukimbia kwa wachapishaji wengine,” asema.

Anasema yeye hukumbana na changamoto nyingi ikiwemo malipo kwa watu wasiomwamini anaweza kufanya kazi yao kwa hali inayostahili.

You can share this post!

Mafuriko yalivyotatiza wakulima Perkerra

Zion Winners wasema coron haitawazuia kutesa ligini