• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 11:33 PM
Kijiji kinachozama kutokana na matimbo

Kijiji kinachozama kutokana na matimbo

RICHARD MAOSI NA KEVIN ROTICH

Wakazi wa kijiji cha Kimolwet eneo la Barut, Kaunti ya Nakuru, wametoroka makwao, baada ya wachimba migodi kufikia makazi yao.

Migodi hiyo inayomilikiwa na watu wenye ushawishi mkubwa serikalini baadhi yao wakiwa ni viongozi, imetapakaa katika kila sehemu ya Kimolwet.
Wachimbaji migodi wamefanya kijiji hicho kuzama katika sehemu moja na kilichobakia ni mahame na nyumba ambazo hazitadumu .
Kulingana na Jane Jebet mkaazi wa Barut anasema kuwa amekuwa akiishi katika sehemu hiyo kwa zaidi ya miaka 10,lakini sasa amelazimika kuhamia kwingine baada ya eneo lenyewe kuwa hatari kwa usalama.
Akizungumza na Taifa Leo Dijitali sehemu ya nyumba yake ilikuwa imechimbika na ilikuwa ikisubiri kumezwa na timbo.
“Wachimba migodi wamekuwa wakilipua mawe kupiti vilipuzi na kusababisha nyumba zetu kuwa hafifu,na hata wakati mwingine huyumbayumba,”akasema.
Jebet anasema tayari mita 10 ya shamba lake imechukuliwa na shughuli yenyewe na anahofia shamba lake lote litapotea ebdapo mambo yataendelea kama yalivyo.
Kabla ya shughuli za uchimbaji migodi kuanzishwa nilikuwa nikimiliki kipande kikubwa cha ardhi lakini sasa mambo yamebadilika.
Sehemu ya shamba lake tayari imebakia kuwa chini ya udhibiti wa wachimbaji migodi wasioonekana kusitisha shughuli zao hivi karibuni.
Aliongezea kuwa eneo hilo limewazika wachimbaji migodi wengi wakiwa katika harakati ya kujipatia kipato.
“Kwa muda mrefu niliokaa hapa nimekuwa nikishuhudia watu wengi wakipoteza maisha yao na wengi wao kiwa ni walevi,”akasema.
Anasema wamekuwa wakituma malalamishi yao kwa idara husika kama vile NEMA na utawala wa mtaa huku wakijaribu kushirikisha  idara husika bila mafanikio.
“Tumekuwa tukipeleka malalamishi yetu katika afisi za kaunti ya Nakuru lakini badala yake huwa hatusaidiki,”Jebet alisikitika.
Mkazi mwingine aliyezungumza na Taifa Leo Dijitali alionyesha nyumba yake ikining’inia katika sehemu ya timbo hilo .
Bi Langat anawalaumu viongozi kwa kuwachochea vijana kuendeleza shughuli zao ingawa wakazi ndio walikuwa wakihangaika.
“Ilinibidi kutafuta sehemu nyingine ya kuishi kwani maisha ndani ya nyumba yangu hayawezi kutabirika,” akasema.
“Wakati mmoja kanisa linalopatikana karibu na eneo la timbo hilo lililalamikia NEMA ,lakini uchimbaji ulisitishwa kwa muda.Isitoshe mgombea wa kiti cha ubunge aliwahi kuwahimiza vijana waendelee kuchimba mchanga na tunashindwa jukumu la NEMA,”alisema.
Kipyegon Kiplangat mkaazi wa hapo karibu anasema anawaonea hurunma watoto wadogo wanaokwenda shuleni kila siku bila uangalizi wa wazazi wao.
“Ninawaonea watoto wa shule huruma wanaopita karibu na timbo asubuhi na mapema wakielekea shuleni,”alisema.
Bw Kiplagat anahimiza NEMA kuingilia kati ili kuokoa maisha ya wakazi wengi na kusaidia wanusuru vipande vyao vya ardhi.
“Wachimbaji migodi ni wenye kiburi na hawapendi kuulizwa jambo lolote kwani wengi wao hudai wapo kazini,”alisema.
Aliomba serikali ya ugatuzi isaidie kutengeneza nafasi nyingi za ajira kwa vijana kwani endapo matimbo yangefungwa vijana wangehangaika.
“Ingawa ni kinyume na sheria matimbo haya yamekuwa yakisaidia kutengeneza nafasi nyingi za ajira kwani vijana wengi wanategemea hapa,” alieleza.
“Serikali kuu na ile ya kaunti zinatakiwa kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuwasaidia vijana wengi wasiokuwa na njia ya kujipatia mkate wa kila siku,” Kiplagat alisema.
Kwa mujibu wa sheria za NEMA 2007, wakazi wanashauriwa kutumia mazingira yao ipasavyo bila kuyaharibu kwani maisha ya baadaye yanayategemea.
“Maelekezo hayo yanazingatia utumiaji wa raslimali za kijamii kwa kuzingatia maisha ya raia wake kwa kuojali maslahi yao,”sehemu ya nakala hiyo ilinukuu.
Lakini cha kusikitisha ni kuwa NEMA kutoka tawi la Nakuru haijapokea malalamishi yoyote kutoka kwa wakazi na walitakiwa kuripoti.
“Tutayaangazia malalamishi hayo kwa kina ili kuhakikisha tunatoa suluhu ya kudumu,”NEMA ilisema.

You can share this post!

Changamoto za mji wa Nakuru katika azma ya kuwa jiji

Kifaa cha kisasa cha kufugia nyuni

adminleo