• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 9:35 PM
KIKOLEZO: Tamu ikizidi sana…

KIKOLEZO: Tamu ikizidi sana…

Na THOMAS MATIKO

WASWAHILI husema tamu ikizidi sana huwa sio tamu tena.

Katika mawazo hayo, ipo ishu ya majeraha ya kooni kwa wanamuziki ambacho ni kitu cha kawaida sana katika maisha yao.

Hutokea mara nyingi msanii anapokuwa kaimba sana na kuishia kuzichosha misuli ya kooni ambayo hulegea, kukwaruzika au kuchanika na kumfanya ashindwe kuimba.

Kitaaluma zaidi, athari yake huwa ni uharibifu wa koromeo inayoishia kuvuruga aina mbalimbali za sauti vipasuo vya mwanamuziki.

Ishu hii huwa nzito kiasi kuwa hata sauti ya msanii inaweza kupotea au hata akashindwa kuzungumza kama kawaida yake.

Na ili kutibu ishu hii, mara nyingi wasanii wameshauriwa na madaktari kutoimba kwa zaidi ya miezi miwili ili kuzipa misulu ya kooni muda wa kutosha kupona.

Kwa walioshiwa kukutwa na majeraha kama haya, wameishia kupoteza dili nyingi. Wafuatao ni baadhi tu wa waathiriwa:

MARIAH CAREY

Nguli wa RnB Mariah Carey naye kawahi kujikuta katika hali hii. Machi 2019 akipiga shoo kule Minneapolis alishtumiwa kwa utumbuizaji duni huku ishu ya sauti yake ikizua mdahalo kutokana na kukosa ule mvuto aliozoeleka nao. Majarida mengi ya burudani yaliripoti kwamba Mariah alitatizika sana kutumbuiza na ilikuwa wazi kwamba alikuwa na tatizo na koo lake.

Katika miaka ya tisini akiwa mwanamuziki machachari, aliachia albamu kadhaa na wakati akiwa kwenye ziara ya utambulisho wa albamu hizo, alishia kupata majeraha mabaya ya misuli ya kooni ambayo katika miaka iliyofuatia, yamemsababishia kuahirisha shoo nyingi.

CELINE DION

Aipatwa na jeraha la kooni Machi 2012 na kulazimika kufutilia mbali shoo kadhaa mjini Las Vegas. Kulingana na kauli yake wakati huo, Celine alisema koo yake ilikuwa imeathiriwa na kirusi na kumwia vigumu kuendelea kuimba.

Baada ya kiuchunguzwa na madaktari, alishauriwa apumzike bila kuimba kwa miezi mitatu

PITSON

Hivi majuzi Pitson kafunguka kwamba amelazimika kuacha kuimba kwa muda wa miezi miwili kufuatia ushauri wa madaktari.

Hii ni kutokana kujeruhi koromeo kwa kuimba sana. Pitson anasema amekuwa akifanya mazoezi sana na kuimba na bendi mfululizo kiasi cha sauti yake kuishia kuwa na mikwaruzo. Mwisho wa siku alishindwa kabisa hata kutoa sauti na sasa anatakiwa kutulia.

“Sitaimba kwa miezi miwili ijayo sababu sauti yangu imeharibika,” akasema.

Anasema inamuumiza moyo kwa sababu hataweza kutengeneza pesa kwa kipindi hicho kwani kuimba ndio ajira yake. Toka alipostaafu kazi ya benki alipovuma na wimbo Lingala ya Yesu, amekuwa akitegemea muziki kujikimu.

“Hakika hiki ni kipindi kigumu sababu sasa sina ajira tena. Nategemea muziki kupata riziki, sijui itakuaje sasa. Sijui nimekosea wapi hadi haya yamenikuta. Sijui ni kuomba siombi sana au ni vipi!” Piston kafunguka.

NYOTA NDOGO

Miaka kadhaa iliyopita kipindi nyota ya Nyota Ndogo ilikuwa inang’aa kupita maelezo kutokana na hiti alizokuwa akiichia mara kwa mara, shoo kibao za nje na ndani ya nchi zilimtembelea.

Kipindi alipoachia hiti yake ya ‘Watu na Viatu’ iliyovuruga chati ya Afrika Mashariki, Nyota Ndogo aliangukia dili kubwa Tanzania ambapo alizunguka nchi hiyo kwa wiki tatu akipiga shoo. Aliporejea nyumbani, hangeweza kuiendelea kuimba kutokana na kupoteza sauti baada ya jeraha ya kooni iliyosababishwa na shoo hizo za muda mrefu.

 

 

Nyota Ndogo anafahamika kwa kibao ‘Subira’. Picha/ Hisani

TEKNO MILES

Novemba 2018 usimamizi wa staa Tekno kutoka Nigeria, ulitangaza kuwa msanii huyo kaamua kuachana na kuziki kwa muda baada ya kupata jeraha la koo kutokana na kuimba sana na shoo nyingi alizofanya.

Jeraha hilo lilianza kumsumbua 2017 lakini akawa analazimisha tu. Ikumbukwe Aprili mwaka huo alilazimika kuahirisha shoo yake Amerika baada ya kulazwa hospitalini kutokana na jeraha la koo.

 

You can share this post!

Arsenal yaziba nyuma EPL iking’oa nanga leo usiku

Kenya Lionesses yaanza kampeni ya kuingia Kombe la Dunia...

adminleo